Tuesday , 3rd Jun , 2014

Michuano ya Taifa ya riadha itakayoshirikisha mikoa yote Tanzania bara na visiwani, inatarajia kuwapa changamoto wanariadha wa Tanzania walioko nje ya nchi wakifanya mazoezi ya kujiandaa na michuano ya madola 2014

Wanariadha wa Tanzania wakichuana katika michuano ya taifa msimu uliopita.

Shirikisho la riadha nchini Tanzania RT linatarajia kuandaa michuano ya ubingwa wa taifa kwaajili ya kupata wachezaji watakaojaza nafasi za wachezaji ambao watakua hawajafikia kiwango katika kushiriki michuano ya madola itakaayofanyika jijini Grascow Scotland

Katibu mkuu msaidi wa RT Ombeni Zavara amesema mashindano hayo yatafanyika jijini Dar es salaam kwa siku mbili kuanzia julai 12 hadi 13 mwaka huu na yatashirikisha mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani

Aidha Zavara ameitaka mikoa itakayoshiriki michuano hiyo kuthibitisha ushiriki wao mapema kabla ya zoezi hilo halijafungwa rasmi june 15 mwaka huu na pia amewataka wawaandae vizuri wanariadha wao ili waje kushindana na si kushiriki.