Friday , 12th Jul , 2019

Wadhamini wakuu wa klabu ya Mbao FC kampuni ya GF Trucks & Equipment Limited imeweka wazi kuwa itaendelea kuidhamini timu baada ya kuzuka tetesi kuwa walitaka kujitoa.

Mbao FC

GF Trucks na Mbao walisaini mkataba wa miaka mitatu ambapo sasa umebaki mwaka mmoja ambao wanaendelea nao huku ukiwa umeboreshwa lakini hawakuweza wazi maboresho hayo.

Mtendaji Mkuu wa GF Trucks, Imrani Karmali amesema bado wana imani na mahusiano mazuri na timu hiyo licha ya kukiri kuwa msimu uliopita haukuwa mzuri kwao.

Nae Mwenyekiti wa Mbao, Solly Njashi ameishukuru kampuni hiyo kwa kuendelea kuwaamini huku akiwahikishia kufanya maboresho kwenye kikosi ili kuongeza ushindani kwenye ligi.