Sunday , 6th Sep , 2015

Pamoja na matokeo ya suluhu ya 0-0 katika mchezo wa jana kwa Stars dhidi ya Nigeria wadau wa michezo kote nchini wameonyesha matumaini kwa kikosi cha stars katika mechi zijazo kama kikosi hicho kitaungwa mkono na kitaandaliwa vizuri.

Kikosi kamili cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars kilichoivaa Nigeria jana.

Wakizungumizia mtanange huo wakuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya mataifa ya Afrika AFCON 2017 itakayofaanyika nchini Gabon wadau hao wamesema kwa kiwango kilichoonyeshwa jana na timu ya taifa astrs katika mchezo huo ni wazi timu hiyo ikipewa nafasi itafanya makubwa zaidi katika siku za usaoni kama hakutakuwa na mabadiliko makubwa katika timu hiyo.

Wakiongea hii leo Mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Mwanza Jackson Songola na mdau wa soka Kaisi Edwin wamesema binafsi wao wameridhishwa na kiwango cha timu hiyo na matokeo ya sare dhidi ya moja ya timu kubwa barani Afrika si jambo dogo hivyo wanapaswa kuungwa mkono na watanzania wote kwa ujumla ili wafanye vema zxaidi ya hapo.

Aidha wadau hao wamesema pamoja na watu wengi kuipa nafasi kubwa Nigeria hasa kutokana na timu hiyo kuundwa na kikosi cha wanandinga wengi wanaocheza nje ya nchi yao tena katika vilabu vikubwa barani Ulaya hilo halikuwazuia Stars inayonolewa na kocha mzawa Boniface Mkwasa kuwahimili Nigeria ambao nao wananolwa na kocha mzawa Sunday Olise na mara kadhaa kuonekana kama Stars ingepata goli lakini kukosekana na umakini wa washambuliaji katika kumalizia nafasi walizopata ukapelekea timu hiyo kupata sare hiyo ambayo ni faida kwa Nigeria ambayo sasa inafikisha alama 4 katika michezo miwili baada ya awali kuichapa Chad mabao 2-0.

Tanzania sasa itahitimisha mechi za mzunguko wa kwanza wa Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 Machi mwakani, itakapoifuata Chad.

Taifa Stars imekamilisha mechi mbili za Kundi G bila ushindi, baada ya awali kufungwa mabao 3-0 na Misri mjini Alexandria Juni mwaka huu, wakati Nigeria inafikisha pointi nne baada ya awali kushinda 2-0 dhidi ya Chad.

Misri wao watakuwa wageni wa Chad Jumapili hii kukamilisha raundi ya pili ya Kundi G. Wote Tanzania na Nigeria wataiombea mabaya Misri Jumapili hii ifungwe ili isipae zaidi katika kundi hilo.

Lakini Misri wanapewa nafasi kubwa ya kushinda na matokeo mabaya sana kwao yanaweza kuwa sare, pamoja na kuwa Chad si timu ya kubeza sana.

Tanzania bado ina nafasi japo finyu ya kwenda Gabon mwaka 2017, iwapo itashinda mechi zake zilizobakia kuanzia ya Machi 25 mwakani dhidi ya Chad.