Thursday , 28th Jul , 2016

Klabu ya Simba imeahidi itawatangaza wachezaji wake wapya na kuwashangaza mashabiki wake siku ya Tamasha la Simba Day.

Rais wa klabu ya Simba Evance Aveva

Tamasha la 'Simba Day' limepangwa kufanyika Agosti 8 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Simba rasmi itawatangaza wachezaji wake wapya wa kitaifa na kimataifa.

Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva amesema watawashangaza mashabaki wao "Itakuwa ni 'suprise', kuna wachezaji ambao watatangazwa na kuwashangaza mashabiki wetu, na kila kitu kinakwenda kwa mpangilio safi kabisa"

"Mashabiki wa Simba waje tuungane kusherekea na kuona kikosi chetu, " alisema Aveva.

Aidha, Aveva alieleza itakavyokuwa wiki ya Simba ambayo itahusisha mambo muhimu kama vile utaoaji damu hivyo viongozi na wanachama mbalimbali wa Simba watachangia damu katika hospitali mbalimbali.

Rais wa Simba, Evans Aveva amesema watafanya hivyo ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya Simba kwenda kusherekea miaka 80 ya klabu hiyo.