Baadhi ya wachezaji na makocha wa mchezo wa tenis katika klabu ya gymkhana jijini Dar es salaam wamepongeza uamuzi wa Rais wa chama cha tenis Tanzania TTA Metusela Mbajo ambaye aliandika barua ya kujiuzuru siku chache zilizopita
Omar Abdalah [china] amesema uamuzi wa kiongozi huyo ni wa busara na wa kukinusuru chama kwani tayari ndani ya chama hicho kulikua na mgogoro wa ndani ambao ulipelekea baadhi ya wajumbe kujiondoa katika chama hicho kitu ambacho kingekua ni kikwazo kwa maendeleo ya tenis nchini
Naye Waziri Rajabu ambaye ni kocha mchezaji wa tenis katika klabu ya Gymkhana amesema kuwa uamuzi ya kujiuzuru kwa Rais ni wazi utagusa mfumo mzima wa uongozi wa chama hicho lakini cha msingi ni kuangalia katiba ya chama hicho inasemaje pindi kiongozi wa juu anapojiuzuru na baadaye utafanyika uchaguzi kumchagua kiongozi wa muda.