Saturday , 28th Nov , 2015

Kocha wa timu ya JKT Ruvu Mrage Kabange amesema, katika Michuano ya Ligi kuu hajaona tatizo la waamuzi katika mechi mbalimbali isipo kuwa ni mapungufu ya timu yake ndio yamechangia timu hiyo kushindwa kufanya vizuri

Kabange amesema, matatizo aliyaona uwanjani baina ya waamuzi na wachezaji ni yakawaida na hata matatizo katika kikosi chake ameshayafanyia kazi tayari kabisa kwa ajili ya muendelezo wa Ligi kuu utakaoendelea Desemba 12 mwaka huu.

Kabange amesema, kwa upande wa nidhamu timu yake inanidhamu kutokana na nitimu ya Jeshi na lazima wawe na nidhamu ili kuweza kufanya vizuri kwani nidhamu pia inachangia mchezaji kuweza kufanya vizuri.