Sunday , 14th Feb , 2016

Venus Williams ametwaa taji la wazi la Taiwan baada ya kumfunga kwa seti mbili Misaki Doi kwa 6-4 6-2, siku ya Jumapili na kuwa taji lake la 49 tangu aanze kucheza mchezo huo wa tenisi.

Venus Williams ametwaa taji la wazi la Taiwan baada ya kumfunga kwa seti mbili Misaki Doi kwa 6-4 6-2, siku ya Jumapili na kuwa taji lake la 49 tangu aanze kucheza mchezo huo wa tenisi.

Williams, mwenye umri wa miaka 35 alitumia saa moja na dakika 26 akimfunga Mjapan huyo kila seti mara tatu.

Williams aliyetolewa raundi ya kwanza kwenye michuano iliyopita ya wazi ya Australia, hakupoteza seti kwenye michuano hiyo iliyokuwa ikipigwa huko mjini Kaohsiung.

Ushindi wa Williams unamuweka kwenye orodha ya kuwa mchezaji wa saba kwa wanawake walioshinda taji hilo la mchezaji mmoja mmoja.