Monday , 6th Apr , 2015

Uongozi wa Timu Shiriki ya ligi kuu soka Tanzania Bara, Polisi Moro umewatimua kambini wachezaji wao sita kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.

Katika taarifa yake, Mwenyekiti wa timu hiyo, Zuberi Seif amesema, wachezaji hao walikutwa na baadhi ya viongozi wa timu hiyo wakinywa pombe usiku wa kuamkia juzi na kupelekea kurudi kambini alfajiri suala lililopelekea uongozi huo kuchukua hatua za kuwatimua wachezaji hao.

Wachezaji waliotimuliwa katika kambi hiyo ni Edward Christopher, Six Mwasekaga, Mussa Mohamed, Jerry Katula na Rogers Gabriel.