Friday , 25th Jul , 2014

Rais wa chama cha mchezo wa gofu kwa wanawake Tanzania TLGU Mbonile Barton amesema hatogombea nafasi yoyote katika uchaguzi mkuu ujao wa viongozi wa chama hicho utakaofanyika katikati ya mwezi ujao mkoani Mororogo

Baadhi ya viongozi wa chama cha gofu kwa wanawake wakishangilia ubingwa.

Zoezi la uchukuaji fomu na urejeshaji fomu kwa wagombea uongozi katika chama cha gofu cha wanawake Tanzania TLGU linaendelea kwa kusuasua wakati siku za kuelekea uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika August 15 mwaka huu zikikaribia

Rais wa TLGU Mbonile Barton amesema fomu zinatolewa bure baraza la michezo nchini BMT na katika matawi ya chama hicho kote nchini na ni fursa sasa kwa wanawake wenye sifa za kukiongoza chama hicho kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama hicho ili waweze kuleta changamoto mpya na kuingiza mawazo yao mapya katika kuhakikisha mchezo wa gofu kwa wanawake unasonga mbele ndani na nje ya nchi kimataifa badala ya kukaa nje na kusubiri kulalamika au kukosoa uongozi ulioko madarakani kwa kile wanachokiona ni mapunguvu.

Aidha Mbonile amesema tangu kuanza kutolewa kwa fomu hizo mwanzoni mwa wiki hii ni mwanamichezo mmoja pekee ndiye aliyejitokeza kuchukua fomu mpaka anazungumza na EATV hii leo.