Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa BMT, Najaha Bakari amesema, uchaguzi huo umepangwa kufanyika Mei tatu mwaka huu ambapo mwisho wa kuchukua fomu hizo ilikuwa ni April 15 lakini wamesogeza mbele ambapo fomu hizo zitachukuliwa mpaka Aprili 30 mwaka huu.
Najaha amesema, nafasi zinazotarajiwa kugombewa katika uchaguzi huo ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti, katibu mkuu, katibu mkuu msaidizi, weka hazina, mweka hazina msaidizi, na nafasi tano za wajumbe ambapo hadi sasa ni fomu saba ndizo zilizochukuliwa.