Monday , 16th Mar , 2015

Kikosi cha Timu ya Taifa ya wanawake Twiga Stars kinatarajia kuondoka Ijumaa ya wiki hii kuelekea nchini Zambia kujiandaa na mchezo wa kufuzu Mataifa Afrika dhidi ya Zambia itakayochezwa Machi 22 mwezi Machi mwaka huu.

Akizungumza na East Africa Radio, Kocha mkuu Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema kikosi hicho kitaondoka kikiwa na wachezaji 18 ambao wamechaguliwa kutoka katika kikosi cha wachezaji 28 walioingia kambini.

Kaijage amesema, Zambia walicheza nao mwaka jana ambao waliwatoa lakini wanaamini wataweza kufanya vizuri kwani wamejiandaa na mazoezi pia yatasaidia katika mchezo huo.