Nahodha wa Timu hiyo John Bocco amesema, wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kukamilisha mechi ya mwisho na watacheza kwa kupambana kwani mashindano hayo yanaumuhimu kwao kwa ajili ya kukijenga kikosi.
Bocco amesema, wamemaliza mazoezi ya mwisho hii leo na wachezaji wenzake wote wapo katika umakini wa kumsikiliza kocha kwa ajili ya kupambana zaidi ili kuweza kufanya vizuri zaidi katika mechi za kimataifa zilizo mbele yao.
Bocco amesema, baada ya kumaliza mashindano hayo wanarejea nchini kwa ajili ya kuendelea na michuano ya Ligi kuu bara ambapo watakutana na Mwadui FC na wanaamini mechi itakuwa ngumu kutokana na kila timu kuweza kuhitaji poinri tatu lakini wao wanasimamia mazoezi waliyopewa na kocha ili kuweza kufanya vizuri zaidi.
Kwa upande wake Nahodha msaidizi wa timu hiyo Himid Mao amesema, wanakutana na timu nzuri na wanaiheshimu lakini wao kama Azam FC watasimamia kile anachowaelekeza kocha kwa ajili ya kuweza kumaliza mashindano hayo wakiwa na rekodi nzuri.
Mao amesema, msimu uliopita walishindwa kufanya vizuri katika mashindano hayo kutokana kutokuwa na uzoefu wa kucheza mechi mfululizo hivyo kwa kipindi hiki wameshakuwa na uzoefu na mashindano.
Mao amesema, mzunguko wa pili ni mgumu kwani kila timu inaenda mwisho hivyo kila timu inapigana ili isiweze kushuka daraja na timu nyingine kupigana kuweza kuchukua ubingwa.


