
Katibu mkuu wa TSA Ramadhan Namkoveka amesema, kamati hiyo itateua wachezaji na makocha wenye vigezo vilivyowekwa ili kuhakikisha timu inafanya vizuri katika mashindano hayo.
Namkoveka amesema, kamati hiyo itasimamia maandalizi ya timu hiyo ili kuhakikisha Tanzania inafanya vizuri katika mshindano hayo.
Namkoveka amesema, wajumbe waliochaguliwa kuunda kamati hiyo ni Leena Kapadia, Invoilata Itatiro, Linges Magesvaran, Michael Livingstone na Alex Mwaipasi.
Mashindano hayo yatazishirikisha timu wenyeji Uganda, Burundi, Djibout, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Somalia, Sudan kusini na Tanzania.