Friday , 6th Feb , 2015

Chama cha mchezo wa Rollball nchini TRBA kinatarajia kukutana mwishoni mwa wiki hii ikiwa ni sehemu ya kujadili mandalizi ya michuano ya AfroAsia yanayotarajiwa kufanyika April mwaka huu nchini Uganda.

Akizungumza na East Africa Radio, Nahodha wa timu ya Taifa ya Rollball Feruzi Juma amesema, kikao hicho kitatoa habari juu ya kinachoendelea katika timu hiyo pamoja na maandalizi mazima kwa ajili ya kuweza kushiriki michuano hiyo.

Feruzi amesema, mpaka sasa timu inaendelea na mazoezi lakini changamoto kubwa inayowakabili ni vifaa suala linalochangia vijana wengi kushindwa kujiunga katika ushiriki wa mchezo huo.

Feruzi amesema, mwaka huu pia wamepata mualiko wa kushiriki michuano ya kombe la Dunia itakayofanyika India mwishoni mwa mwaka huu nchini India ambao utashirikisha nchi 54.