
Mabingwa wa kombe la dunia timu ya TSC ya Tanzania
Mabingwa wa dunia wa michuano ya soka kwa watoto wa mitaani Timu ya soka ya Tanzania hii leo wamefanyiwa hafla fupi ya kupongezwa mara baada ya kuwasili nchini wakitokea jijini Rio De Jeneiro nchini Brazil walikotwaa kombe hilo kubwa, baada ya kuchuana nchi zaidi ya 15 toka nchini tofauti duniani.
Katika hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es salaam serikali iliwakilishwa na mkurugenzi wa michezo toka wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bi. Juliana Yasoda ambaye ametoa wito kwa taasisi mbalimbali kuangalia watoto wa mitaani katika michezo yote kwani wameonesha wanaweza kuiletea sifa Tanzania.
Naye Rais wa kituo hicho cha michezo kwa watoto wa mitaani Altaf Hiran ametoa shukarani kwa serikali kwakuwa imewaunga mkono kwa wakati wote, Jambo lililowaletea mafanikio katika michuano hiyo.
Kwa upande wake kocha mkuu wa kikosi hicho Suleiman Jabir akiongea na EATV amesema ushindi wa vijana hao ni maandalizi mazuri waliyoyapata, nidhamu na kufuata maelekezo yake huku kipa wa kikosi hicho ambaye ni Kipa bora wa michuano hiyo Emmanuel Amos naye akiunga mkono kauli hiyo huku akikiri kuwa mashindano yalikuwa magumu mno.
