Tuesday , 25th Aug , 2015

Kikosi cha timu ya Taifa cha vijana wenye umri chini ya miaka 15 kimeingia kambini kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya kombaini ya Morogoro mwishoni mwa wiki hii.

Kikosi hicho kinachonolewa na kocha wake Bakari Shime, kinatarajiwa kucheza michezo miwili na timu ya kombaini ya Morogoro jumamosi na jumapili mjini Morogoro, ambapo kocha huyo amekua akitumia nafasi hiyo kupima uwezo wa vijana wake na kuboresha kikosi kwa kuongeza vijana wengine anaowaona wanafaa katika timu hiyo.

Timu hiyo ya vijana wenye umri chini ya miaka 15, inajandaa na kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 17 nchini Madagascar mwaka 2017.