Afisa habari wa Shirikisho la soka nchini TFF Alfredy Lucas amesema, kamati ya ufundi chini ya Mkurugenzi Salum Madadi ipo katika maandalizi kwa ajili ya kutaja kikosi kitakachoingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo huo.
Lucas amesema, katika mashindanoi hayo timu 14 zitashiriki katika mchujo huo ambapo kila nchi shiriki itacheza na timu moja ili kufuzu ikiwa ni mchezo wa nyumbani na ugenini.
Alfredy amewataka wadau mbali mbali kujitokeza kwa ajili ya kusaidiana na TFF ili kuiwezesha timu hiyo kufanya maandalizi mazuri ambayo yatawawezesha kusonga mbele katika fainali hizo.



