Tuesday , 17th Mar , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni inatarajiwa kuondoka siku ya alhamisi kuelekea jijini Cairo nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa soka la ufukweni utakaofanyika siku Jumapili

Tanzania inapaswa kupata ushindi katika mchezo wa marudiano dhidi ya Misri ili kufuzu kwa fainali za soka la ufukweni barani Afrika zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli kufuatia kupoteza mchezo wake wa awali uliofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.

Msafara wa timu ya Beach Soccer, utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Ahmed Msafiri Mgoyi, kocha mkuu John Mwansasu, kocha msaidizi Ali Sheikh Alhashby, meneja Deogratius Baltazar na daktari wa timu Dr Leonidas Rugambwa.

Wachezaji ni Rajabu Chana Kipango, Ahmed Rajab Juma, Roland Revocatus Kessy, Samwel Sarungi Opanga, Feisal Mohamed Ussi, Mohamed Makame Silima, Mwalimu Akida Hamad, Juma Sultan Ibrahim, Kashiru Salum Said na Ally Rabby Abdallah.