Mcheza gofu wa Marekani,Tiger Woods, amejitoa kwenye mashindano ya US PGA, na atakosa kwa mara ya kwanza mataji yote manne makubwa ya kalenda ya mwaka, tangu mwaka 1995.
Woods, mwenye umri wa miaka 40, hakucheza shindano lolote karibu mwaka sasa, baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutibu tatizo la mgongo mwaka uliopita.
Wakala wake, Mark Steinberg, amethibitisha kuwa, Woods, hatocheza kwa kwa msimu uliobaki, kwa kuwa hayupo tayari kwa kwa mashindano.





