Monday , 14th Dec , 2015

Imesemekana kuwa kukosekana kwa fedha na uwekezaji finyu kwa klabu za hapa nchini ndiko kunakopelekea uhaba wa vituo vya kulelea vipaji vya vijana wanaochipukia.

Tigana lukinja wa pili kutoka kulia mwenye jezi nyeupe kwenye kikosi cha Majimaji ikiwa ni mechi yake ya kwanza ya ligi kuu katika maisha ya mpira walipocheza na simba sport mwaka 2001.

Akizungumza na East Africa Radio mkurugenzi wa kituo cha Njombe Sports Academy ambaye pia ni kocha Tigana Lukinja amesema klabu nyingi nchini zimekosa uwezo wa kifedha lakini pia watu wenye weredi wa kutafuta fedha hizo ambazo zingesaidia kujenga vituo hivyo.

Tigana maarufu kamaTeacher ambaye alichezea klabu za Tukuyu Stars ya Mbeya,,Nazareth ya Njombe,Majimaji ya Ruvuma,Lipuli ya Iringa na Mtibwa sugar amesema ni vigumu kupata klabu bora zitakazotuwakilisha vyema kwenye michuano mikubwa ngazi ya klabu barani Afrika kama hatutathamini soka la vijana.

Pia amesema endapo viongozi wa klabu hizi wataacha dharau kwa nyota vijana wanaochipukia basi klabu hizi zitafanya vizuri na pia kujenga timu ya Taifa nzuri inayotokana na vijana hao ambao wanauwezo wa kucheza soka nje ya nchi.