Friday , 27th Mar , 2015

Timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) tayari imewasili leo jijini Mwanza majira ya saa sita mchana, ikiwa na kikosi chake kamili kwa ajili ya mchezo dhidi ya Taifa Stars siku ya Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Malawi imewasili ikiwa na kikosi chake kamili cha wachezaji 18 wakiwemo wachezaji saba wanaocheza soka la kulipwa katika nchi za Afrika Kusini, Congo DR, Msumbuji na Zimbabwe.

Wachezaji wa kimataifa waliowasili ni nahodha Joseph Kamwendo wa TP Mazembe Congo DR, Chimango Kayira wa Costal de Soul ya nchini Msumbiji, Frank Banda HBC Songo ya Nchini Msumbiji, Esau Kanyenda Polokwane City ya Nchini Afrika Kusini, Harry Nyirenda wa Black Leopards ya Nchini Afrika Kusini, Limbikani Mzava wa Celtic ya Afrika Kusini) Gerald Phiri wa Caps United ya Zimbambwe)

Wegine ni McDonald Harawa wa Hoyale FC, Richard Chipuwa wa Wanderers, Lucky Malata wa Silver, John Lanjesi wa Civo, Francis Mulimbika wa Wanderers, John Banda (Blue Eagle), Earnest Tambwe (Surestream) , Micium Mhone (Blue Eagle), Chikoti Chiriwa (Red Lions), Peter Wadabwa (Silver) na Amos Khamula(Support Ballaton).

Mkuu wa msafara ni Alexander Waya, Kocha mkuu Young Chimodzi, kocha msaidizi Jack Chamangwana, kocha wa makipa Pillip Nyasulu, Daktari wa timu Levison Mwale, Meneja wa timu Frank Ndawa na Afisa Habari James Sangala.

Kikosi cha timu ya Taifa ya Malawi kinatarajiwa kufanya mazoezi leo saa 10 jioni katika uwanja wa CCM Kirumba, huku siku ya Jumamosi wakipata nafasi ya kufanya mazoezi tena kwenye uwanja huo wa mchezo.