Monday , 20th Apr , 2015

Chama cha Mpira wa Magongo nchini THA kimetakiwa kuwasilisha matatizo yahusuyo mchezo huo mapema ili kuweza kupatiwa ufumbuzi mapema.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel amesema serikali ipo kwa ajili ya kuboresha michezo mbalimbali hapa nchini ikiwa ni pamoja na uboreshwaji wa vifaa vya michezo hiyo.

Gabriel amesema, pamoja na serikali kusaidia mchezo huo, pia jamiii inatakiwa kujitokeza kwa ajili ya kusaidia ili uweze kufanya vizuri katika mashindano ya ndani na nje ya nchini na kuitangaza nchi katika ramani ya michezo.

Kwa upande wake mwenyekiti wa THA, Abraham Sykes amesema ili kuboresha zaidi na kuukuza mchezo huo hapa nchini, wanaendelea na mafunzo ya mchezo huo kwa wanafunzi wa shule za Dar es salaam na Mtwara ambapo Mikoa ya Arusha, moshi na Tanga wapo katika mpango wa kuanza kutoa mafunzo katika shule za mkoa huo ili kuweza kupata wachezaji wengi zaidi ambao ni vijana.