Thursday , 1st May , 2014

Chama cha mpira wa magongo Tanzania THA hii leo kimeanza kutoa mafunzo katika shule ya sekondari ya makongo ya jijini Dar es salaam ukiwa ni mpango mkakati wa chama hicho katika kuhakikisha mchezo huo unakua na kuenea kote nchini.

Baadhi ya wachezaji wa mpira wa magongo wakipambana

Chama cha mpira wa magongo Tanzania THA hii leo kimeanza kutoa mafunzo katika shule ya sekondari ya makongo ya jijini Dar es salaam ukiwa ni mpango mkakati wa chama hicho katika kuhakikisha mchezo huo unakua na kuenea kote nchini.

Katibu mkuu msaidizi wa THA Mnonda Magani amesema shule ya sekondari Makongo ni mwanzo wa safari yao katika kukuza mchezo huo hapa nchini kupitia shule mbalimbali

Kwa upande wake, mkufunzi wa mpira wa magongo nchini kocha Valentina Quaranta maarufu kama arobaini amewataka wadau, wadhamini na watanzania wote kwa ujumla wenye uwezo kusaidia vifaa vya mchezo huo katika shule ili kufanikisha azma ya chama hicho

Aidha Valentina amesema bado wana upungufu wa vifaa pamoja na msaada wa vifaa vichache alivyopata kutoka kwa wachezaji wa zamani wa nchini Italia.

Tags: