Akizungumza na East Africa Radio, makamu mwenyekiti wa TGU, Joseph Tango amesema, tayari wameanzisha timu za vijana ambao wanapewa mafunzo ya muda mrefu kwa ajili ya maandalizi ya mshindano hayo.
Tango amesema, TGU imelazimika kuanzisha timu maalumu za vijana katika Klabu ya Gymkhana ya Dar es salaam, Arusha, Kagera, Morogoro na mikoa mingine ili kuwapatia mafunzo ya muda mrefu yatakayoweza kuwajengea msingi imara kabla ya kushindana kimataifa.
Tango amesema, mazungumzo katika vyama vya kimataifa vya Gofu ya kuomba ushiriki katika mashindano ya Olimpiki yanaendelea vizuri na kuna uwezekano mkubwa mchezo huo ukawa miongoni mwa michezo itakayoshiriki michuano ya Olimpiki Rio 2016.