Rais wa shirikisho la soka Tanzania TFF Jamal Malinzi akitangaza kusimamisha uchaguzi wa klabu ya Simba.
Shirikisho la soka nchini TFF limesimamisha kwa muda mchakato wa uchaguzi wa klabu ya soka ya Simba ambao uchaguzi wake ulikua ufanyike june 29 mwaka huu,
Rais wa TFF Jamal Malinzi amesema uamuzi huo ni kutokana na TFF kupokea malalamiko kadhaa juu ya ukiukwaji wa maadili wa wagombea na wanachama kadhaa wa klabu ya simba,
Malinzi amesema kwa mujibu wa katiba ya simba ibara ya 16 kifungu 1[i] na ibara ya 30 kifungu [h] kamati ya utendaji ya Simba inaagizwa iunde kamati ya maadili mara moja
Kwaupande mwingine rais Malinzi amesema TFF inaiagiza klabu ya Simba hadi kufikia june 30 mwaka huu iwe imeshakamilisha zoezi la kuunda kamati ya maadili, kusikiliza mashauri yatakayoletwa mbele yake na kuyatolea maamuzi haraka
Aidha Malinzi amesema kwamujibu wa kanuni za uchaguzi wa TFF Ibara ya 2 kifungu cha [4] kamati ya utendaji ya Simba SC itaendelea kuwa madarakani hadi hapo mchakato wa uchaguzi wa Simba SC utakapokamilika.