
Afisa habari wa TFF Baraka Kizuguto amesema, timu hiyo ambayo imewasili hapo jana ikitokea nchini Afrika Kusini baada ya kumaliza kambi yake ya siku 10 ili kuwa katika mazoezi ya kujituma huku wakiwa na morali ya hali ya juu kwa ajili ya kuipeperusha vizuri bendera ya Tanzania katika kuwania tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia.
Kizuguto amesema, tiketi kwa ajili ya mchezo huo zitaanza kupatikana hapo kesho katika vituo vinavyotumika katika uuzwaji wa tiketi za mechi mbalimbali za ligi kuu jijini Dar es salaam huku akiwataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuipa sapoti timu hiyo.