
Telela akisaini mkataba kuitumikia Ndanda FC ya Mjini Mtwara
Awali kulikuwa na taarifa kwamba Telela angeacha sokana na kurejea darasani kujiendeleza kielimu.
Afisa habari wa klabu hiyo Idrisa Bandali amesema Telela amesaini mkataba wa mwaka mmoja, huku dau la usajili wake linabaki kuwa siri kati ya mwajiri na mwajiriwa kama yeye mwenyewe alivyotaka iwe.
Telela aliachwa na klabu ya Yanga baada ya mkataba wake kumalizika na kocha wa klabu hiyo Hans van Pluijm huku akisesemakasema mchezaji huyo hayuko katika mipango yake katika msimu ujao.