
Wawakilishi wa Tanzania Kimataifa
Yanga Sc ambao ni mabingwa watetezi wa ligi kuu ya NBC 2024-2025 inacheza leo Jumamosi saa 10:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki mchezo wa pili hatua ya awali ikiwa ni mchezo wao wa kwanza ugenini dhidi ya Silver Strikers mjini Lilongwe,Malawi. Kuelekea mchezo huo Kocha mkuu wa Yanga Sc "Romain Folz" anaamini maandalizi waliyofanya yanatosha kuwapa matokeo chanya dhidi ya wapinzani wao.
Huku Azam FC na KMKM zote kutoka Tanzania zitashuka dimbani Saa 10:15 jioni visiwani Zanzibar, Kwa upande wa KMKM wamekiri kuwa wametimiza azma yao kubwa ya msimu huu huku upande wa Azam kocha Florent Ibenge anaisaka rekodi ya kwanza kwa timu hiyo kucheza hatua ya makundi michuano ya CAF.
Kila la kheri wawakilishi wa Tanzania katika michuano hii mikubwa ngazi za vilabu barani Afrika.