Akizungumza na East Africa Radio, Kocha wa Timu ya Tanzania, Nassoro Sharrif amesema michuano hiyo ambayo ni sehemu ya kufuzu kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika Rio de Janeiro, Brazil mwaka 2016 ilishirikisha nchi za Kenya, Burundi na wenyeji Tanzania ambapo Kenya Pia imechukua nafasi ya pili kwa wanaume na Burundi imechukua nafasi ya pili kwa upande wa wanawake.
Sharrif amesema, michuano hiyo imekuwa na changamoto kwa upande wa Tanzania ikiwemo maandalizi suala ambalo limekuwa ngumu kuanza maandalizi mapema kwa ajili ya kushiriki mashindano hayo ambayo ni makubwa kwa upande wao.
Sharrif amesema, timu ya Taifa ya Tanzania imekaa kambi ya siku tano tofauti na timu kutoka nchi shiriki suala lililochangia wachezaji kushindwa kufanya maandalizi mapema japo sehemu za kufanyia mazoezi zipo nyingi na zinatosha kwa ajili ya maandalizi lakini kilichoikwamisha ni kambi kwa ajili ya timu kukaa pamoja ikiwa ni sehemu ya maandalizi ni sehemu nzuri ya maandalizi