Monday , 16th Feb , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni jana imeibuka na ushindi wa mabao 5- 3 ugenini dhidi wa wenyeji timu ya Taifa ya Kenya kwenye mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa fukwe za jijini Mombasa.

Katika mchezo huo mabao ya Tanzania yalifungwa na Ali Rabbi mabao manne na Kipindi cha kwanza kilimazika kwa Tanzania kupata mabao 2 Kenya 1, kipindi cha pili kilimalizika Tanzania 4 Kenya 3 na kipindi cha tatu na cha mwisho kwa mchezo kumalizika kwa Tanzania kupata mabao 5 Kenya 3.

Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa Jumamosi wiki hii Februari 21, 2015 jijini Dar es salaam, na endapo timu ya Taifa ya Tanzania itafanikiwa kuwatoa Kenya, itacheza na timu ya Taifa ya Misri katika hatua inayofuata.

Mchezo wa kwanza utafanyika kati ya tarehe 7 na 8 Machi 2015 jijini Dar es salaam na marudiano yatafanyika nchini Misri kati ya tarehe 13 na 14 Machi 2015 ambapo timu inarejea leo jijini Dar es salaam ikitokea jijini Mombasa nchini Kenya.