Tanzania ilifuzu hatua ya pili baada ya kuiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya mabao 12 -9, na endapo itafanikiwa kuwatoa Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika visiwa vya Shelisheli mwezi April mwaka huu.
Waamuzi watakaosimamia mchezo huo ni Eid Haitham Eid Hassan kutoka nchini Sudan huku akisaidiwa na mwamuzi wa kwanza Abaker Mohamed Bilal kutoka nchini Sudani na mwamuzi msaidizi wa pili akiwa Abdallah Hassan Hassaballa mtunza muda akiwa ni Boubaker Bessem kutoka nchini Tunisia wakati kamisaa wa mchezo huo akiwa ni Khiba Herbert Mohoanyane kutoka nchini Lesotho.
Mchezo wa marudiano kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania na Misri unatarajiwa kufanyika nchini Misri kati ya Machi 20, 21 na 22 mwaka huu.