Tuesday , 4th Mar , 2014

Kikosi cha Taifa Stars kesho kinataraji kujitupa katika uwanja wa Sam Nujoma jijini Windhoek, Namibia kwa ajili ya mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya wenyeji Namibia (Brave Warriors) inayofundishwa na kocha Ricardo Mannetti.

Afisa habari wa TFF Boniface Wasmbura amelazimika kutoa ufafanuzi juu ya kauli ya awali kwamba kikosi cha Taifa Stars kilichopo chini ya Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi ambaye ana leseni A ya ukocha inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kwamba kilichaguliwa na shirikisho hilo

Wambura amesema kuwa kiukweli kikosi cha timu hiyo kilichaguliwa na kocha Madadi na ilitangazwa awali kuwa TFF ndio imefanya uteuzi huo kutokana na kwamba walikua hawajavunja mkataba na kocha Kim Palsen.