Tuesday , 17th Jun , 2014

Taifa stars inatarajia kwenda nchini Botswana kwaajili ya kambi ya wiki mbili ili kuwakabili timu ya taifa ya Msumbiji, The Mambaz.

Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania taifa stars.

Timu ya taifa ya Tanzania taifa stars inataraji kwenda nchini Botswana kwaajili ya kambi ya mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa kwanza wa raundi ya pili kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Afrika dhidi ya Mambaz ya Msumbiji mchezo ambao utapigwa Julai 20 mwaka huu jijini Dar es salaam.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kambi hiyo ni pendekezo la benchi la ufundi la stars lengo likiwa ni kuhakikisha timu hiyo inapata maandalizi ya kutosha na wao kama TFF kwa sasa wanaendelea kushughulikia maandalizi ya kambi hiyo.

Aidha Wambura amesema lengo la TFF ni kutimiza mahitaji yote muhimu na mapendekezo ya benchi la ufundi ili kuhakikisha timu hiyo inavuka raundi hiyo ya mwisho na kuingia hatua ya makundi na baadaye kutwaa tiketi ya kwenda Morocco ambako ndiko kutafanyika fainali za michuano hiyo ya AFCON hapo mwakani.