Monday , 10th Nov , 2014

Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limesema kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania taifa stars kilichochini ya kocha mkuu mholanzi Mart Nooij na msaidizi wake mtanzania Salum Mayanga kimekusanyika hii leo na kufanya mazoezi ya pamoja huku

Kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania [Taifa Stars]

Wachezaji 22 kati ya 24 wakikosi cha timu ya taifa ya Tanzania taifa stars wameingia kambini leo nakufanya mazoezi katika viwanja vya gymkhana jijini Dar es salaam

Akizungumza na eatv mkurugenzi wa mashindano wa TFF Boniface Wambura amesema stars wanajiandaa na mechi ya kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) dhidi ya Swaziland itakayochezwa Novemba 16 mwaka huu jijini Mbabane

Wambura amesema wachezaji wawili wanaocheza klabu ya TP Mazembe ya DR Congo Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu hawatakuja nchini na badala yake watakwenda moja kwa moja jijini Johanesbury nchini Afrika kusini ambako wataungana moja kwa moja na kikosi hicho ambapo baadae wachezaji hao watarejea katika timu yao wakati wenzao wakirudi jijini Dar es salaam kujiandaa na michuano ya challenge

Aidha Wambura amesema kesho asubuhi kikosi hicho kinataraji kwenda jijini Johanesburg Afrika kusini kuweka kambi rasmi ya siku nne kwaajili ya mchezo huo na michuano ya challenge ambayo hatima yake bado haijajulikana baada ya waliokua wenyeji kwa mwaka huu nchi ya Ethiopia kujivua uenyeji wa michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya taifa

Kikosi cha wachezaji wote 24 walioitwa na vilabu wanavyotoka katika mabano ni ni pamoja na makipa Aishi Manula (Azam) na Deogratias Munishi (Yanga).

Mabeki ni Abubakar Mtiro (Kagera Sugar), Aggrey Morris (Azam), Emmanuel Simwanda (African Lyon), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga), Nadir Haroub (Yanga), Osacr Joshua (Yanga), Said Moradi (Azam), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Shomari Kapombe (Azam).
 
Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Haruna Chanongo (Simba), Himid Mao (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Said Ndemla (Simba) na Salum Abubakar (Azam).
 
Washambuliaji ni Juma Luizio (ZESCO, Zambia), Mbwana Samata (TP Mazembe, DR Congo), Mrisho Ngasa (Yanga), Simon Msuva (Yanga) na Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DR Congo).