Wednesday , 26th Aug , 2015

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na Libya siku ya Ijumaa kwenye moja ya viwanja vilivyopo mjini Kartepe, Uturuki.

Taifa Stars na Libya zote zimeweka kambi nchini humo kujiandaa na mechi za kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika na usiku wa Ijumaa zitamenyana katika mchezo wa kirafiki.

Katika taarifa yake, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa anatarajiwa kuutumia mchezo huo kukipima kikosi chake kwa mara ya kwanza nchini humo, baada ya mazoezi ya siku nne.

Mkwasa amesema huduma na vifaa vilivyopo katika eneo walilofikia wanavyotumia kwa ajili ya mazoezi ni vizuri, hivyo ratiba yake ya mazoezi inakwenda kama alivyopanga katika maandalizi ya wiki moja ya kujiandaa na mchezo dhidi ya Nigeria.