Soka la Algeria limekumbwa na kashfa ya utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu,baada ya mchezaji wa kimataifa wa nchi hiyo Youcef Belali na wachezaji wengine watatu kufungiwa.
Taarifa zinasema kuwa kumbi za usiku zimekuwa zikitumiwa na wachezaji kutumia madawa ya kuongeza nguvu, wakiwa na imani ya kuwa imara wanapokuwa uwanjani.
Wataalamu wa afya wamelielezea gazeti la El-Khabar kuwa soka la Algeria lipo kwenye machafuko tangu vilabu vya nchi hiyo kutokuwa na madaktari na viongozi wake kuendekeza rushwa.
Waandishi wa habari za michezo nchini humo wanailaumu serikali na shirikisho la soka kwa kushindwa kusimamia rushwa na utumiaji wa dawa.
Bado serikali na shirikisho la soka nchini Algeria havijasema lolote juu ya kashfa hiyo ya utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu kwa wachezaji.
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limemfungia Belaili anayekiputa kwenye klabu ya USM Alger kwa miaka miwili kutojishughulisha na soka ndani na nje ya nchi, huku baadhi ya wachezaji wengine wakifungiwa hadi miaka minne huku uchunguzi ukiendelea.





