Thursday , 21st Jan , 2016

Kocha mkuu wa kikosi cha Timu ya Taifa, Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa amesema hajapata taarifa rasmi ya aliyekuwa nahodha wa kikosi hicho Nadir Haroub Cannavaro kustaafu kukitumikia kikosi hicho.

Mkwasa amesema, Cannavaro bado yupo kwenye mipango yake ya timu ya taifa ya Tanzania na hata kama ameshafikia hatua hiyo si vizuri kuzungumza kwasababu amekuwa akizungumza muda mrefu na maamuzi yatakuwa yamebaki kama yalivyofikiwa.

Mkwasa amesema, anayaheshimu maamuzi ya Cannavaro na kwake bado ni mchezaji mzuri kwani amekaa naye na nikiongozi mzuri katika kuhamasisha vizuri na bado anamuhitaji lakini alichokifanya ni mabadiliko ya kawaida tu kwenye timu kwakuwa alimuamini anaweza.

Mkwasa amesema, amesikia kuwa ameshastaafu kuitumikia timu ya taifa lakini hata kama kustaafu lazima astaafu kwa heshima na lazima wafanye utaratibu na yeye kama kocha atasimamia utaratibu wake ili waweze kuandaa ni namna gani aweze kupata heshima ya kustaafu kwake.

Cannavaro alitangaza kustaafu soka la kimataifa akipinga utaratibu uliotumika kumuondoa katika unahodha wa timu na kumkabidhi Mbwana Samatta na kusema yeye kama nahodha hakupewa taarifa rasmi ya kubadilishiwa majukumu zaidi ya kupata raarifa hiyo kupitia vyombo vya habari, hivyo kwake ilikuwa ni kudharauliwa.