Monday , 21st Mar , 2016

Beki wa Azam FC Shomari Kapombe amesema, hana mpango wa kuwania kiatu cha mfungaji bora kwa msimu huu bali anaangalia zaidi kuiweka timu yake katika nafasi nzuri.

Beki wa Azam FC, Shomary Kapombe

Kapombe amesema, kumsikiliza zaidi kocha na kuangalia anahitaji nini pamoja na juhudi zake binafsi ndivyo vilivyofanikisha kufikia malengo ya yeye kuweza kufunga katika mechi mbalimbali za Ligi kuu ya Soka Tanzania bara.

Kapombe anashikilia nafasi ya tisa akiwa na Magoli saba aliyofunga katika mechi za Ligi kuu huku Hamis Kiiza wa Simba SC akiongoza kwa kuwa na magoli 19 ya Ligi.