
Wachezaji wa Simba wakiwa mazoezini
Simba imefanya mazoezi chini ya kocha Joseph Omog akisaidiana na msaidizi wake, Jackson Mayanja ambao kwa pamoja wameonesha kubadilika kwa kuifanya timu yao icheze kwa kushambulia zaidi.
Katika mechi iliyopita, Simba iliichapa Majimaji FC kwao Songea kwa mabao 3-0, magoli yaliyofungwa na Ibrahim Ajibu, Said Ndemla na Laudit Mavugo.
Simba kwa sasa inashika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 48 nyuma ya Yanga wanaoshikilia usukani kwa pointi 49, huku timu zote zikishuka dimbani mara 21.