Saturday , 29th Mar , 2014

Shirikisho la soka nchini TFF limesema kuwa mpaka sasa ni klabu ya Simba pekee ndio iliyowasilisha marekebisho ya katiba yake.

Boniface Wambura-Afisa Habari TFF

Shirikisho hilo lilitoa agizo kwa wanachama wake wote, kuhakikisha kabla ya Machi 20 mwaka huu wanafanya marekebisho katika katiba zao, kwa kuingiza kipengele cha kamati ya maadili.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kuwa marekebisho hayo ni agizo la shirikisho la vyama vya soka ulimwenguni FIFA kwa wanachama wake wote kufanya marekebisho hayo