
Waziri Nape akikagua uwanja baada ya kutokea uharibifu huo, mwezi Oktoba mwaka jana
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ndiye aliyeamua kuufungulia uwanja huo na kuruhusu vilabu vya Simba na Yanga kuendelea kuutumia uwanja huo ikiwemo matukio mengine ya kijamii kuanzia leo tarehe 27, Januari, 2017 kwa kufuata taratibu zilizopo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali wa wizara hiyo Zawadi Msalla, Waziri Nnauye amefikia uamuzi huo baada ya kuridhika na ukarabati wa miundombinu ya uwanja huo uliofanywa na vilabu vya Simba na Yanga.
Nape pia amewatahadharisha wapenzi wa michezo kutunza mali za serikali kwa manufaa ya watanzania wote na kusisitiza kuwa hatua kali zitachukuliwa siyo tu kwa vilabu bali pia kwa muhusika mmoja mmoja kwa msaada camera mpya za usalama zilizofungwa uwanjani hapo.
Hali ya uwanja wa huo mara baada ya uharibifu, mwezi Oktoba mwaka jana
Vilabu hivyo vilifungiwa kuutumia uwanja huo Mwezi Oktoba mwaka jana mara ya mchezo kati yao, uliomalizika kwa uharibifu mkubwa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na viti kung'olewa na mageti kuvunjwa.
Mbali na kuvifungia, serikali pia ilizuia mapato ya vilabu hivyo, na kuviamuru kuufanyia ukarabati, ambapo kwa pamoja vilabu hivyo vilifanya ukarabati na kisha kuomba msamaha vikiiomba serikali iviruhusu kuutumia.