Wednesday , 16th Mar , 2016

Uongozi wa klabu ya soka ya Simba umesema nidhamu kwa klabu hiyo ambayo sasa inanolewa na Mganda Jackoson Mayanja ni suala la kwanza na hakuna mtu yeyote aliye juu ya klabu hiyo na wanajipanga kwa sasa kuhakikisha haki ya klabu hiyo inalindwa.

Aliyekuwa nahodha wa Simba menye kitamba mbele Hassan Isihaka akishangilia na wenzake katika moja ya michezo ya timu hiyo.

Klabu ya Simba, imetangaza kumsimamisha kwa mwezi mmoja beki wake wa kati kinda Hassan Isihaka.

Pamoja na kumsimamisha beki huyo kisiki mwenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na washambuliaji wasumbufu, pia imetangaza kumvua unahodha msaidizi pale atakaporejea kundini.

Hii ni kutokana na madai ya kumjibu kwa lugha isiyo ya kiungwana Kocha wake, Jackson Mayanja alipotaka kumpanga acheze katika mechi ya Kombe la FA dhidi ya Singida United.

Hayo yamesemwa leo na Msemaji wa Simba, Haji Manara wakati alipozungumzia suala la utovu wa nidhamu lililokuwa likimkabiri Isihaka ambaye alisimamishwa kwa muda usiojulikana.

Uamuzi huo wa kumsimamisha ambao ni sehemu ya uamuzi wa kamati ya utendaji, huenda ukasababisha Isihaka kuokosa Ligi Kuu Bara.

Siku Manara alipotangaza kumsimamisha Isihaka kwa muda usiojulikana, mshambuliaji wa Simba, Hamisi Kiiza aliandika mtandaoni kwamba mchezaji huyo alikuwa anaonewa na kuchafuliwa jina.

Lakini siku iliyofuata, isihaka alimuabisha Kiiza kwa kuomba radhi kutokana na kosa la kuzungumza kwa lugha isiyo ya kiungwana mbele ya kocha wake na wachezaji wengine.

Uongozi wa Simba ukampa onyo pia na kumtaka azikanushe habari hizo ambazo zilionekana zinalenga kutetea watovu wa nidhamu.

Kwa upande mwingine klabu ya soka ya Simba imetangaza rasmi kutoendelea na michezo mingine ya ligi kuu ya soka Tanzania bara mara baada ya mchezo wao wa jumamosi dhidi ya wenyeji wa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga Coastal Union hii ni kutokana na kile wanachodai kuwa ni kubadilika kwa mara kwa mara kwa ratiba ya ligi hiyo na kuziacha timu za Yanga na Azam wanaoshindania nao ubingwa wakiwa na idadi ya mechi nyingi mkononi maarufu kama viporo kitu ambacho wao kama Simba wamekitafsiri kama ni hujuma za wazi za kupanga matokeo na hata bingwa.

Mkuu wa idara ya habari ya timu hiyo Haji Manara amesema wamestukia mchezo huo mchafu na sasa wametangaza rasmi mara baada ya mchezo wao dhidi ya Coastal Unio basi hawatashuka dimbani mpaka pale wapinzani wao hao watakapo cheza michezo yao ya viporo na timu zote kuwa na michezo sawa.

Wakati huo huo uongozi wa klabu ya Simba umetanga kuwa utawasilisha rasmi barua ya malalamiko yao kwa waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo kulalamikia vitendo vya shirikisho la soka nchini TFF kuchelea ama kupuuza kusikiliza na kuchuakua hatua malalamiko mbalimbai ya klabu hiyo.

Mkuu wa idara ya habari ya timu hiyo Haji Manara amesema wamefikia uamuzi huo baada ya kugundua kuna njama za wazi na kupuuzwa kwa klabu hiyo na chombo hicho kikubwa cha maamuzi katika soka kwani tangu mwaka jana waliwasilisha malalamiko juu ya usajili wenye utata wa kiungo mshambuliaji wa timu hiy Ramadhan Singano [mesi] kwenda Azam fc, lakini pia mwaka huu waliwasilisha madai mengi likiwemo suala la mkuu wa idara ya habari ya watani wao Yanga Jerry Muro kudaiwa kutamka maneono yasiyofaa kwa klabu hiyo na pia yeye binafsi.

Akimalizia Manara amesema hata tumia njia za kielekroniki kupeleka barua hiyo kwa waziri ambayo nakara yake pia itakwenda TFF ni kwamba atapeleka mwenyewe kwa mkono ili kujihakikishia barua hizo zimefika kwa walengwa na zifanyiwe kazi haraka iwezekanavyo ili kurudisha heshima ya mchezo wa soka hapa nchini ambao amedai umeingiliwa.