Msimu uliopita, Yanga waliandika historia kwa kuwashangilia Simba ilipotoa sare na Azam. Sare hiyo ilirahisisha ubingwa kwa Yanga.
Mchezo wa kwanza ni Mbeya Derby kati ya Mbeya City na Tanzania Prisons utakaopigwa katika uwanja wa sokoine Mbeya. Mchezo huu ni upinzani wa jadi.
Mchezo mwingine ni kule katika uwanja wa mkwakwani Tanga baina ya mabingwa watetezi Yanga dhidi ya wenyeji Mgambo Shooting mchezo ambao Yanga inahitaji ushindi ili iweze kuifukuza Azam fc inayoongoza ligi hiyo na Mgambo inahitaji ushindi ili iepuke kikombe cha kushuka daraja.
Na mchezo mwingine ni ule ambao unatazamwa kama ndio wenye maamuzi ya nani ataukaribia ubingwa pale Azam FC watakapowaalika Simba katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Kuelekea mchezo huo afisa habari wa timu ya Simba Asha Muhaji amesema kuwa wamejipanga vizuri kuhakikisha wanaibuka na ushindi hapo kesho na pia amekanusha taarifa za kuwa timu hiyo imepewa fedha na Azam ili wafungwe.