Afisa michezo wa baraza la michezo Tanzania BMT Richard Mganga ambao ndio watasimamia zoezi hilo la uchaguzi amesema kuwa kila kitu ama taratibu zote zimekamilika likiwemo suala la usaili ambao umefanyika hii leo
Aidha Mganga amewakumbusha wajumbe na kuwataka wajumbe wa mkutano huo kuhakikisha wanakuja na viambatanisho vyote ambavyo vitawawezesha kuwa na sifa ya kupiga kura hapo kesho.
