Friday , 29th Apr , 2016

Kocha wa Timu ya Taifa ya vijana Serengeti boys Bakary Shime amesema, anaangalia uwezekano wa kuweza kupata mechi nyingine ya kirafiki ambayo itamsaidia kujua viwango vya wachezaji wake kabla ya kuelekea nchini India katika mashindano.

Shime amesema ameanza mazoezi rasmi hii leo na vijana wake baada ya juzi na jana kuwa katika zoezi la kufuatilia paspoti pamoja na vipimo vya MRI kwa vijana hao.

Shime amesema, anaangalia muda uliopo kwa ajili ya maandalizi na ataangalia kama kunauwezekano wa kupata mchezo wa kirafiki lakini sio lazima sana kwani kwa sasa anaanglia zaidi uwezo wa vijana wake ambao wanajiandaa kwa ajili ya mashindano nchini India.