Afisa TRA Horohoro - Edwin Lwato
Bidhaa hizo zimekamatwa katika oparesheni maalum inayofanywa katika vijiji tofauti vilivyopo mpakani ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mtandao wa kihalifu unaojihusisha na uingizaji wa dawa za kulevya, wahamiaji haramu na ukwepaji wa kodi kwa serikali.
Wakizungumza katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania timu ya watendaji wa Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), maafisa uhamiaji na wakaguzi wa mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA tawi la Horohoro, wamesema lengo la oparesheni hiyo ni kuhakikisha kuwa mipaka ya nchi inakuwa salama.
kuhusu kukamatwa kwa dawa za kulevya Mrakibu Mwandamizi Msaidizi wa idara ya uhamiaji nchini tawi la Horohoro Mwesiga Lubalila amesema katika zoezi la kukabilianana uingizaji wa bidhaa haramu, kundi la watu waliokuwa na pikipiki zilizokuwa zimebeba maboksi walipobaini mtego wa kukamatwa walilazimika kuzitupa pikipiki hizo na kisha kukimbia.
Amesema maafisa hao walipopekua na walikuta dawa za kulevya aina ya mirungi zenye uzito wa kilo 98 iliyokuwa imefungwa katika vifurushi vyenye uzito wa kilo moja moja kila kimoja..
Kufuatia hatua hiyo mkaguzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa Thomas Nkondola amesema bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nchini kenya hazitaruhusiwa kuingia endapo kama hazijafanyiwa ukaguzi kufuatia baadhi ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa zilizopitwa muda wake na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji





