Friday , 10th Apr , 2015

Serikali na jamii kwa ujumla imeombwa kujitokeza kwa ajili ya kuweza kuisaida kambi ya timu ya taifa ya ngumi za wanawake inayotarajiwa kuingia kambini Mei 15 mwaka huu ikijiandaa na mashindano ya Olimpiki mwakani.

Akizungumza na East Africa Radio, Mjumbe wa maendeleo ya wanawake Shirikisho la ngumi za Ridhaa nchini BFT, Aisha George amesema timu hiyo yenye mabondia wapatao 11 wataanza mazoezi kwa kuungana na timu ya wanaume ambapo zote zitakuwa kambi ya muda mrefu.

Aisha amesema, pia kambi hiyo imepata mualiko katika nchi za Congo Brazavile na Serbia ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwakani kushiriki mashindano ya Olimpiki.