Kikosi cha Serengeti Boys
Serengeti Boys imeweka kambi jijini Antananarivo, Madagascar kujiandaa na mchezo dhidi ya Afrika Kusini katika mchezo wa awali kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika utakaofanyika Agosti 6 mwaka huu nchini Afrika Kusini.
Mara baada ya mchezo dhidi ya Afrika kusini timu ya Serengeti Boys itarejea nchini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa marudiano utakaofanyika Agosti 21, mwaka huu Uwanja wa Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Wachezaji walioko kambini ni pamoja na makipa, Ramadhani Kabwili, Kelvin Kayego na Samwel Edward Brazio.
Kwa upande wa mabeki wako Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Israel Mwenda, Dickson Job, Ally Msengi, Issa Makamba na Enrick Nkosi.
Viungo ni KelvinbNaftal, Ally Ng’anzi, Asadi Ali Juma Ali, Syprian Mtesigwa, Ibrahim Ali na Shaban Ada, huku washambuliaji wakiwa ni Mohammed Rashid, Yohana Mkomola na Muhsin Makame.
Serengeti Boys inakwenda kucheza na Afrika Kusini baada ya kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa.
Mshindi wa jumla kati ya Serengeti Boys na Afrika Kusini, atacheza na timu mshindi kati ya Namibia na Congo-Brazaville.







