Tuesday , 23rd Oct , 2018

Baada ya nyota wa mieleka duniani Roman Reigns kutangaza kuwa anaumwa Saratani, shirikisho la mchezo huo duniani WWE limempa pole na kuweka wazi kuwa hatashiriki tena fainali ya kuwania mkanda wa dunia.

Roman Reigns akiwa na mkanda wa ubingwa wa dunia.

WWE wamethibitisha kuwa mwanamieleka  huyo anaumwa saratani ya damu yaani 'Leukemia' inayoshambulia chembechembe nyeupe za damu.

Roman mwenye miaka 33 kwa sasa ndiye anayeshikilia mkanda wa dunia wa mchezo huo, alizungumza katika jukwaa na kusema kuwa  hatashindana kugombea mkanda huo ila atarejea baadaye iwapo  afya yake itaimarika.

Kwa mujibu wa bosi wa WWE, Vince McMahon mkanda wa dunia sasa utawaniwa na wanamieleka wawili tu badala ya watatu ambao ni Brock Lesnar na Braun Strowman, Novemba 2, mwaka huu.

Roman ambaye alijiunga na mieleka mwaka 2010, amesema aligundulika kuwa na Saratani hiyo aina ya Leukaemia akiwa na miaka 22, na amekuwa kwenye wakati mgumu hivyo kufikia maamuzi ya kuchukua mapumziko ili aendelee na matib