
Wachezaji wa Tottenham na Man United kwenye mechi ya jana usiku.
Tottenham imeshinda mara tatu tu katika uwanja wa Old Traford, katika mechi zote za ligi ilizowahi kushinda dhidi ya United na michezo yote wameshinda wakiwa chini ya makocha wapya, ushindi wake wa kwanza ilikua ikisimamiwa na Andre Villas-Boas mwaka 2012, wapili ikiwa na Tim Sherwood mwaka 2014, pamoja na Mauricio Pochettino mwaka huu.
Iliwachukua sekunde 133 tu sawa na Dakika mbili na sekunde 13 kuandika magoli mawili na kufanya huo ndio muda wa haraka zaidi kwa timu hiyo kufunga magoli mawili katika uwanja wa ugenini mara ya mwisho walifanya hivyo mwaka 2012 waliposhinda dhidi ya Everton kwa mabao ya Nikica Jelavic pamoja na Steven Pienaar.
Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Tottenham Harry Edward Kane amefunga magoli 25 katika viwanja 28 vya Premier league akiwa hajafunga katika viwanja vitatu, Upton Park unaotumiwa na West ham United, The Stadium of Light unaotumiwa na Sunderland, pamoja na Cardiff City Stadium uwanja wa timu inayotoka Wales ya Cardiff.
Lakini Pia kipigo hicho cha Mbwa koko kwenye Uwanja wa nyumbani kimeifanya Manchester United kupoteza mechi mbili za mwanzo katika mechi tatu za ufunguzi kwa mara ya kwanza Tangu walivyofanya hivyo miaka 26 iliyopita katika msimu wa mwaka 1992-93 lakini pamoja na kipigo hicho katika msimu huo waliweza kuibuka kuwa mabingwa wa ligi hiyo .
Ila pia hiki ni kipigo chake cha 50 katika uwanja wake wa nyumbani katika historia ya Manchester United.
Licha ya hayo kwa Upande wa Kocha wa United, José Mário dos Santos Mourinho Félix, hiki ni kipigo chake cha kwanza kikubwa katika uwanja wa nyumbani tangu aanze historia yake ya ukocha katika mshindano yote aliyowahi kusimamia lakini pia hii ni mara ya kwanza kwa kocha huyo kupoteza michezo miwili kati ya mitatu ya mwanzo ya msimu katika maisha yake yote ya ukocha.